Polisi Dodoma imewakamata Wafanyabiashara wa kukopesha hela.

Polisi Dodoma imewakamata Wafanyabiashara wa kukopesha hela.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kushikirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo na kuwachukulia hatua stahiki kwa kuwafikisha katika vyombo vya Sheria. Kamanda Mallya ametoa wito huo leo Mei 8,2024

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kushikirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo na kuwachukulia hatua stahiki kwa kuwafikisha katika vyombo vya Sheria.

Kamanda Mallya ametoa wito huo leo Mei 8,2024 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

“Kama mnavyofahamu kuna kampeni ya Jeshi la Polisi inayoendelea katika jiji la Dodoma ya familia yangu haina mhalifu mashuleni,vyuoni na katika nyumba za ibada ikiwa na lengo la kutoa elimu ya masuala ya ulinzi na usalama kwa makundi Yote”amesema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya akizungumza na wanahabari leo Mei 8,2024 katika kituo cha Polisi Central (Picha na Manase Madelemu)
Aidha amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Machi hadi Aprili,2024 Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kufanya.

Operesheni,misako na doria katika maeneo tofauti ya jiji la Dodoma na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 120 wa uvunjaji,Uporaji na ukabaji na kufanikiwa kuokoa mali mbalimbali

“Kupitia Operesheni, misako na doria hizo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kuwakamata wafanyabiashara wanaoendesha biashara ya ukopeshaji fedha kwa wananchi maarufu kama Kausha damu kinyume na Sheria ya watoa huduma ndogo ndogo za fedha daraja la pili ya mwaka 2028″amesema

Kamanda Mallya amewataja watuhumiwa waliokamatwa katika Operesheni hiyo ni Adrian Alchard Gervas ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Logic Microcredit Company Mali ya Merry Alchard Gervas ambaye ni mkazi wa Dodoma anayeendesha biashara ya ukopeshaji maeneo ya chadulu A kata ya Tambuka Reli.
Amemtaja mwingine kuwa ni Fatuma Said Ally mfanyakazi wa kampuni ya Brown Finance Company Ltd mali ya Pius Steven Mushi mkazi wa Dodoma naye anaendesha biashara ya ukopeshaji maeneo ya Makole jirani na Chuo cha Biashara (CBE) Dodoma.

“Watu hawa wamekuwa wakifanya biashara hii kinyume na Sheria ambazo zimewekwa viwango vya riba anavyotakiwa kulipa mkopaji ni asilimia 3.5 lakini wafanyabiashara hawa wamekuwa wakiwalipisha wakopaji wao kiasi cha asilimia 20 hadi 40 kwa mwezi huku wakiwataka kuwa na marejesho ya kila siku”amesema

Pia amesema kuwa dhamana ya mikopo hiyo ni vitu na mali mbalimbali ambavyo vinamilikiwa na mkopaji kama samani za ndani (Vitanda,Godoro, TV,Music system vyombo vya kupikia,Pikipiki na Magari

Kamanda Mallya amesema kuwa Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Jfive Team
ADMINISTRATOR
PROFILE

Posts Carousel

Translate »